Louis Oosthuizen Ajiondoa Kwenye Mashindano ya Masters

Mchezaji wa golf kutoka nchini afrika kusini na bingwa wa mwaka 2010 kwenye mashindano ya wazi Louis Oosthuizen amejiondoa kwenye mashindano ya Masters kutokana kupata majeruhi ambayo mpaka sasa haijafamiki ni nini zaidi kinamsumbua.

Louis Oosthuizen ambaye anashika nafasi ya 14 kwa wacheza golf bora duniani alikuwa akicheza na mshirika wake Tiger Woods, ambaye ataendelea kushiriki michuano hiyo baada ya kurejea kutoka kwenye ajari ya gari aliyopata miezi kumi na nne iliyopita.

Louis Oosthuizen anaungana na muingereza Paul Casey ambaye alijitoa kwenye  mashindano hayo siku ya Jumatano kabla ya mashindano kuanza siku ya alhamisi, lakini anagekuwa kwenye kundi lingine tofauti na kundi la Woods.

Oosthuizen ameshika nafasi za pili kwenye michuano sita mikubwa, ikiwemo mwaka jana kwenye mashindano ya US Open na PGA Championship,  na alishika nafasi ya tatu kwenye michuano ya British Open na pia alishawai kushika nafasi ya pili kwenye michuano ya Masters mwaka 2012.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

Acha ujumbe