Rory Mcllroy ameondoa ukame wa kubeba mataji baada ya kuibuka kidedea kwenye mashindano ya Wells Fargo Champions kwa mara ya 3.

Ni wiki 6 tu zimepita, tangu Rory aanzekufanya kazi na kocha Pete Cowen na matunda yameanza kuonekana. Bingwa huyu namba 15 kwenye mchezo wa gofu duniani, aliibuka kidedea baada ya kupiga shuti moja la umbali wa mita 68 na kunyakua taji hilo

Mara ya mwisho kwa Mcllroy kubeba taji ilikuwa mwaka 2019. Akizungumza baada ya ushindi huo, Mcllroy amesema “Inapendeza, ni kama muda mrefu umepita tangu nimeshinda. Dunia imebadilika sana kutoka ilivyokuwa, sasa hivi kila mtu ameathirika na janga hili – COVID19.

Mcllroy, Mcllroy Bingwa Wa Wells Fargo Championship, Meridianbet

“Kwangu maisha yamebadilika sana, sasa hivi ni baba,nimeshinda siku ya Wanawake, namfikiria Erica (mke wangu) na mama yangu kule nyumbani.

“Hili ni moja ya maeneo ninayoyapenda duniani. Kuondoa ukame kwa kushinda hapa tena, inapendeza. Inapendeza kucheza mbele ya mashabiki kwa mara nyingine.”

Abraham Ancer alimaliza katika nafasi ya 2 huku Victor Hovland na Keith Mitchell wakimaliza kwenye nafasi ya 3.


PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Mcllroy, Mcllroy Bingwa Wa Wells Fargo Championship, Meridianbet

CHEZA HAPA

4 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa