Kocha wa Simba Sc, Didier Gomez asema anaamini huu ni wakati sahihi wa kurudi kileleni mwa msimamo wa ligi kuu bara, VPL.

Akizungumza na Mshikemshike ya Azam Tv, Gomez amedai kwamba timu yake itarejea kwenye nafasi ya kwanza mapema kwa kushinda mechi zao zote za viporo. Simba inashika nafasi ya tatu ikiwa na alama 46, ikipishana na kiongozi Yanga Sc ambaye ana alama 51 huku akiwa amecheza michezo minne zaidi ya Simba.

Katika mahojiano hayo pia, Gomez alipongeza jitihada zilizooneshwa na wachezaji wake katika hatua ya makundi ya kombe la klabu bingwa Africa. Asema kundi lilikuwa gumu lakini kikosi chake kilijitoa sana na kuhakikisha wanashinda mechi zote ziwe za ugenini au nuyumbani.

Simba imefuzu robo fainali ya michuano hiyo huku ikitarajiwa kukutana na moja kati ya timu hizi tatu, Kaizer Chiefs ya Afrika kusini, MC Alger au CR Belouizdad zote za Algeria.

Akielezea mipango yao kuelekea mechi hizo, kocha huyo Didier amesema kwamba anaamini kikosi chake kipo kwenye nafasi nzuri na wanawaheshimu wapinzani wao na wapo tayari kukutana na yeyote yule na watacheza kwa tahadhari. Simba itajua timu itakayokutana nayo pale droo ya robo fainali itakapopigwa tarehe 30 mwezi huu.

Simba inategemewa kucheza mechi zao nne za viporo hivi karibuni, ikianza na mechi kati yao na Mtibwa Sugar hapo kesho katika Uwanja wa Mkapa saa moja usiku.


JILIPE KWA NAMBA ZAKO ZA BAHATI NA KENO

Kila mtu ana namba zake za bahati, Meridianbet tunatambua namba zinaweza kukufanya milionea leo. Jilipe kwa namba zako za bahati kila baada ya dakika tano.

gomez, Gomez: Tunarudi Kileleni Mapema Tu!, Meridianbet

CHEZA HAPA

6 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa