Baada ya kufunga goli la kusawazisha na kuwapatia Manchester United ahueni ya kuingia kwenye nafasi ya 4 katika msimao wa Ligi Kuu UingerezaEPL . Kinda Mason Greenwood anaendelea kuonesha uwezo wake wa kupachika magoli.

Greenwood amekuwa na msimu bora ndani ya kikosi cha Ole Gunnar Solskjaer msimu huu akizifumania nyavu mara 17 katika michuano yote. Goli lake dhidi ya Westham United ni goli la 10 kwenye Ligi Kuu Uingereza –EPL msimu huu.

manchester united, Greenwood: Nyota Inayong’ara Manchester United, Meridianbet

Japokuwa kinda huyu aliongelewa na Solskjaer tangu wakiwa katika maandalizi ya msimu mpya kule Australia ambapo Solskjaer alisema Greenwood ni mfungaji mahiri. Kinda huyu hakupata nafasi ya kuichezea Manchester United mpaka ilipofika mwezi Disemba mwaka jana ndipo alipopata nafasi yake ya kwanza kuitumikia United katika EPL.

Historia inasema, tangu kuanzishwa kwa Ligi Kuu Uingereza – EPL mwaka 1992. Ni Michael Owen pekee ndio kinda aliyefikisha magoli mengi (18) akiwa katika umri mdogo. Romelu Lukaku alifunga magoli 14 msimu wa mwaka 2012-13 wakati Wayne Rooney alifunga magoli 11 msimu wa mwaka 2004-05.

manchester united, Greenwood: Nyota Inayong’ara Manchester United, Meridianbet

Hakuna mchezaji kinda mwingine ambaye amewahi kufunga magoli mengi kwenye michuano yote katika msimu mmoja ndani ya kikosi cha Manchester United kama Greenwood aliyefunga idadi ya magoli (17) sawa na George Best mwaka 1965-66, Brian Kidd mwaka 1967-68 na Wayne Rooney mwaka 2004-05.

Katika mchezo kati ya Manchester United dhidi ya Westham United. Mason Greenwood alipata 66% ya kura za mchezaji bora wa mechi zilizopigwa na mashabiki wa Manchester United. Greenwood aligusa mpira mara 49, alitoa pasi 38, alipiga  mashuti 3 na alifunga goli 1. Mechi hii ikiwa ni mechi yake ya 50 akiitumikia Manchester United.

manchester united, Greenwood: Nyota Inayong’ara Manchester United, Meridianbet

Mchezo wa kumaliza msimu utawakutanisha Manchester United dhidi ya Leicester City ambapo United anahitaji ushindi au suluhu ili amalize katika nafasi 4 za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Uingereza – EPL na hivyo kufuzu kushiriki michuano ya UEFA msimu ujao.

 


Kwa sababu ya thamani ya pesa yako, kwa kila muamala unaofanya wa kuweka pesa kwenye akaunti yako ya Meridianbet unapata 5% bonasi.

Soma hapa zaidi

51 MAONI

  1. Mchezo wajana ulikuwa nzuri sana kwa west ham walionyesha kuwa wako vizuri Manchester united waliponea chupu chupu kufungwa na sasa wanatamba kwa kutoka sare nakuwazidi magoli Chelsea kwa sasa

  2. Hii ipo poa sana kwa sababu Greenwood anajituma sana na kila mechi anafanya poa hii ndio inafanya aanze kwa kila mechi now

  3. Mchezo wa kumaliza msimu utawakutanisha Manchester United dhidi ya Leicester City ambapo United anahitaji ushindi au suluhu ili amalize katika nafasi 4 za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Uingereza – EPL na hivyo kufuzu kushiriki michuano ya UEFA msimu ujao.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa