Antoine Griezmann anatajwa kuwa na hamu ya kurejea Atletico Madrid msimu huu wa joto.

Rais wa Barcelona Joan Laporta amethibitisha kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa anapatikana sokoni kwa uhamisho msimu huu wa joto wakati klabu hiyo ikisaka kuweka sawa vitabu vyao vya fedha.

Mshindi wa Kombe la Dunia amehusishwa na kurejea Atletico kama sehemu ya makubaliano ya kubadilishana na nyota Sauli Niguez, lakini mabingwa wa La Liga wameshindwa kufikia makubaliano na kikosi cha Ronald Koeman.

Kwa mujibu wa Sport, Griezmann yuko tayari kuondoka Camp Nou kwenye soko la sasa, lakini mshambuliaji huyo ana nia ya kuhamia Atletico Madrid.

Wakala wa Griezmann Awasiliana na Timu za EPL

 

Ripoti hiyo inadai kwamba vilabu kadhaa vya Ligi Kuu Uingereza na Serie A viko tayari kumchukua kwa mkopo kwa kampeni ya 2021-22, na kipengele cha uhamisho wa kudumu msimu ujao wa joto.

Mfaransa huyo alifunga mabao 133 na kutoa asisti 50 katika mechi 257 za Atletico kati ya mwaka 2014 na 2019 kabla ya kuhamia Barcelona kwa dili la pesa nyingi.

Griezmann amejitahidi sana kuonyesha kiwango chake bora huko Camp Nou, akiweza kufunga mabao 35 na asisti 17 katika mechi 99 za klabu kwenye mashindano yote.


FURAHIA KASINO MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Kasino ya Mayan Eagle inakukufanya kuwa bingwa wakati wowote unapoamua kuicheza. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa