Kocha Mkuu wa timu ya Manchester City, Pep Guadiola amesema ya kuwa walipambana sana kwa umoja na ndio jambo ambalo liliwafanya wao kutinga kwenye hatua ya fainali ya kombe la ligi ya Mabingwa la UEFA.

Ushindi wa mabao 2- 0 dhidi ya PSG walioshinda kwenye nusu fainali ya pili iliochezwa jana, imewafanya watinge kwenye fainali za UEFA kwa jumla ya mabao 4-1.

Guadiola vs PSGMagoli hayo 2 yaliofungwa na mchezaji Riyad Mahrez kwenye dakika ya 11 na 63 katika uwanja wa nyumbani wa Manchester City huku mshambuliaji Angel Di Maria wa PSG alipewa kadi nyekundu kwenye dakika ya 69.

Guadiola-Man-city

Kutangulia kwa Manchester City kwenye fainali za UEFA kunawafanya wasubiri mchezo kati ya Chelsea dhidi ya Real Madrid utakaochezwa leo katika uwanja wa nyumbani wa Chelsea, Stamford Bridge majira ya saa 4:00 usiku.

Guardiola amesema:”Tulipambana kwa pamoja na kujituma, hili nina amini kwamba ni neno ambalo ninaweza kusema, kutinga kwetu hatua ya fainali ni jambo la furaha,” .

Je, Guardiola na timu yake watafanikiwa kutwaa ubingwa wa UEFA mwaka huu?


TENGENEZA FAIDA KUPITIA MCHEZO WA TITAN DICE UKIWA NA MERIDIANBET KASINO

Unapokuwa kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, huna sababu ya kucheza kwa mashaka. Titan Dice, ni mchezo unaweza kukupatia mamilioni kwa mzunguko mmoja!

guadiola, Guadiola Asema Kilichowabeba Dhidi ya PSG, Meridianbet

SOMA ZAIDI

16 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa