Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola amekiri na kusema imekuwa rahisi kwake kushinda mataji kutokana na kufundisha klabu kubwa katika kazi yake ya ukocha.

Guardiola ameshinda taji lake kubwa la 25 katika maisha yake ya ukocha wakati Aymeric Laporte akiwaangamiza Tottenham dakika za jioni katika dimba la Wembley.

“Ni vizuri. Nilikuwa katika vilabu vikubwa: Barcelona, ​​Bayern Munich, na hapa. Ndio sababu ni rahisi kufanya,” Guardiola aliiambia Sky Sports baada ya kuulizwa juu ya mafanikio yake katika ukocha.

 

Man City Guardiola

 

Meneja huyo pia alizungumzia juu ya mashabiki kuruhusiwa Wembley kwa kiwango kidogo kwa mara ya kwanza kikosi chake kilicheza mbele ya mashabiki baada ya miezi kadhaa.

“Hakukujaa [uwanjani] lakini kulikuwa kelele kubwa [kutoka kwa mashabiki],” akaongeza

“Leo tunafurahi sana kuwa tunapata taji la nne mfululizo katika mashindano haya. Tulijaribu kushinda mchezo, tukatengeneza nafasi nyingi.

“Walikuwa na nafasi kadhaa [Tottenham] kwenye kaunta lakini kwa ujumla tulikuwa na mchezo mzuri.” aliongeza Guardiola.


KWANI MERIDIANBET WANASEMAJE! MKWANJA UPO KWENYE KASINO MPYA YA MINI POWER ROULETTE.

Unawezaje kukosa ubingwa ndani ya kasino hii maridhawa, Nafasi ya kushinda mkwanja ni kwa kila mtu, Meridianbet inakupa nafasi ya kuwa mmoja ya washidi leo, unasubiri nini?

Mini Power Roullete

CHEZA HAPA

12 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa