Meneja wa Man City, Pep Guardiola anasema kuwa akifikisaha umri wa miaka 72 basi ataenda Italia, atakuwa mkufunzi na kumualika Roberto Baggio kuwa msaidizi wake.

Roberto Baggio na Guardiola walicheza pamoja kule Bresci, na bosi huyu wa City anaamini kuwa wanaweza kuwa pamoja sasa kwenye ukufunzi ikiwa atakuwa kocha wa timu ya taifa ya Italia.

Guardiola Anafurahia Mechi Yake ya 700 Wikendi Hii.

Akizungumzia historia yake na Baggio, anasema enzi zao bwana huyu aliweza kucheza nafasi yeyote, na haikuwa rahisi kumshawishi staa huyu wa zamani kuondoka Italia, Serie A. Kwa mujibu wa Guardiola wachezaji bora walipatikana Italia na kila mtu alipenda kucheza Italia.

Akizungumzia nia yake miaka Ijayo anasema, anatarajia kwenda kuwa mkufunzi Italia, pale anapofikisha umri wa miaka 72.

Nikiwa na miaka 72 na kuja kuwa kocha wa Italia, nitamuomba (Baggio) kuwa msaidizi wangu. Nitajaribu kumrejesha kwenye ulimwengu wa soka. Lakini hauwezi kumshawishi Bagio, yeye hufanya maamuzi.”

 

-Pep Guardiola


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

kane, Kane Aweka Wazi Maazimio Yake Kucheza UEFA., MeridianbetBASHIRI SASA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa