Klabu ya Tottenham Hotspur inatarajia kumleta Milan Skriniar klabuni hapo katika dirisha lijalo la uhamisho la msimu wa joto, licha ya uwezekano wa kuwa na ushindani mkubwa. Mourinho anaonekana kuwa na hamu kubwa ya kuinasa saini yake.

Skriniar alikuwa anahusishwa sana na mpango wa kumalizana na Inter Milan msimu uliopita, baada ya kuonekana amepoteza radha na kukosa nafasi ya mara kwa mara kwenye kikosi kilichoanza. lakini hata hivyo, staa huyu amekuwa shemu muhimu ya kikosi cha Antonio Conte msimu huu akiwa amecheza jumla ya mechi 30 kwenye michuano yote.

Milan Skriniar
Milan Skriniar

Kwa mujibu wa mwandishi wa Italia, Fabrizio Romano, Spurs walitoa ofa ya ada ya euro milioni 30 msimu uliopita, kiasi ambacho kilikuwa kidogo zaidi ya kiasi walichokihitaji waitaliano. Kwa mujibu wa mtangazaji huyu, Spurs sasa watahitaji kulipa ada ya euro milioni 60 ikiwa wamepania kuinasa saini ya Skrinia katika dirisha lijalo.

Mourinho anaripotiwa kuwa anamkubali sana Skriniar, na angetamani awe sehemu ya kikosi chake. Taarifa zinasema kuwa Spurs walikuwa karibu sana kuinasa saini yake, isipokuwa walijifungia kwenye ofa yao ya ero milioni 30 kati ya euro milioni 42.5 ambayo Inter Milan waliiweka kama dau la kuanzia.

Klabu zingine ambazo tayari zimehusishwa na staa huyu ni Manchester United na Manchester City.


 

UNAWEZAJE KUKOSA KASINO YA BREAK AWAY LUCKY WILDS INAYOKUPA NAFASI YA USHINDI MURUA.

Break Away Lucky Wilds ni moja ya Sloti pendwa katika kasino za #meridianbet inayokupa mara 11,000X ya dau lako, unayo nafasi ya kuwa milionea unasubiri nini?

Skriniar, Hamu ya Maurinho Kumleta Skriniar Tottenham, Meridianbet

CHEZA HAPA

7 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa