Kuna kitu kimoja Harry Kane kwa sasa anahitaji. Anahitaji kuamua anataka akumbukwe kama nani. Moja ya wachambuzi wakubwa wa soka tanzania Edo Kumwembe alisema, anatakiwa kuchagua kuwa shetani au malaika.

Miezi mitatu ijayo atakuwa na miaka 28. Kama anahitaji kuondoka Spurs, huu ndio muda sahihi. Hana muda mwingine.

Harry Kane
Harry Kane

Abaki Spurs awe gwiji wa milele? Au aondoke Spurs akavae medali. Hili la pili linaonekana kuwa ‘la maana’ zaidi.

Kwa inavoonekana, Spurs haina dalili ya kuwa timu tishio kwa miaka ya usoni. Kama anataka medali, lazima akubali kuwa msaliti, aondoke katika timu iliyomlea.

Kwenye mkataba wake Harry Kane, amebakiza miaka mitatu na Spurs. Kwa maana hiyo timu itakayomsajili itahitaji kuvunja benki kuilipa Spurs.

Kama utamwaga pesa nyingi kwa ajili ya Kane, labda ukalipa pauni 150 milioni, basi utahitaji misimu minne bora kutoka kwake. Je Harry Kane atakuwa katika ubora huu misimu minne ijayo??

Harry Kane
Harry Kane

Lakini pia timu atakayoenda, inapaswa kuwa timu ambayo imeshajengwa, Kane aende kukamilishaa tu. Timu ambayo ina uhakika wa kupigania kombe. Hayupo katika umri ambao anatakiwa asubiri timu itengenezwe. Ni timu ngapi zilizokwisha tengenezwa zinamuhitaji Kane??

Spurs wanaweza kumshawishi abaki kwasababu ana mkataba wa muda mrefu, Lakini yeye mwenyewe yupo tayari kubaki?? Ana kiu ya medali na Spurs haionekani kumpatia ‘Medali Kubwa’ siku za usoni.

Mwisho wa siku, suala la Harry naliona ni gumu sana. Kuondoka Spurs ni ngumu na kubaki Spurs ni ngumu. Tusubiri muda utoe hukumu.


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

Harry Kane, Harry Kane Achague Kubaki Ama Kuondoka Spurs, MeridianbetBASHIRI SASA

5 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa