Baada ya kuwepo kwa fununu za muda mrefu juu ya kocha wa zamani aliyefanya makubwa na klabu ya Arsenal kwa wakati ule, Arsene Wenger kuanza kuhusishwa na kujiunga na klabu ya Bayern ambayo hadi sasa haina kocha mkuu kwenye safu ya uongozi wake wa kiufundishaji yaliibuka mengi kwamba huenda mtu sahihi kupewa nafasi hiyo alikuwa ni huyo Mzee Wenger ambaye ameweza kuonekana kama yupo karibu sana na klabu hiyo na hata aina ya soka ambalo linachezwa na klabu hiyo halima utofauti kabisa na lile ambalo Wenger alikiwa akilifundisha alipokuwa na Arsenal.

Masuala ya kimfumo kwa hakika yasingeweza kumpa shida yoyote Wenger kwa sababu kile alichokifanya akiwa mkufunzi alikuwa anakirejesha katika klabu hiyo. Uchezaji wa pasi nyingi na kasi ya kushambulia ulikuwa ni aina ya mfumo wa Wenger japo kwake hakuwa na mashambulizi ya kulazimisha kama yale ya City, huenda kutokana na viungo aliokuwa nao.

Taarifa za kwamba kocha huyo angeweza kuifunza klabu hiyo zimeondoshwa kwa sasa na hazipo kabisa, kinachoangaliwa ni kuendelea kwanza na kocha aliyepokea mikoba kutoka kwa Kovac ambaye aliondoshwa na uongozi wa klabu hiyo kutokana na mwenendo wa matokeo wa klabu hiyo.

Wenger ameweza kujichomoa kabisa kwa kusema hakuwahi kukaa chini na uongozi wa klabu hiyo wakajadili juu ya yeye kuifundisha klabu hiyo. Kwanza hajafikiria kabisa kuwa Meneja wa klabu hiyo kwa sasa. Kwa siku za usoni hatazamii kabisa kuwa sehemu ya uongozi klabuni hapo, anachokiangalia kwa sasa ni kuendelea na mapumziko yake ya ukufunzi akiamini ni wakati ambao yupo huru zaidi.

Hans Flick ndiye aliyekaimu nafasi ya Kovac ndani ya klabu hiyo na huenda akiendelea na matokeo ambayo ameyaanza dhidi ya klabu hiyo mwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya ikaweza kumpeleka mbele zaidi na kuchukua nafasi hiyo.

Bayern ni klabu kubwa ambayo inahitaji kocha mwenye jina ili kuweza kuijenga zaidi. Uwepo wa makocha wakongwe huwa na chachu ya kuchochea ubingwa ndani ya klabu husika kwa sabahu ni masuala ya kirekodi.

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa