Dean Henderson amekubali kuongeza mkataba wake wa mkopo kutoka Manchester United kubakia Sheffield United hadi mwisho wa msimu. Alitakiwa kurudi Old Trafford mnamo Juni 30, lakini ameruhusiwa kubaki huko Bramall Lane kwa mechi zao saba za mwisho za ligi.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 amekuwa katika fomu nzuri kwa The Blades msimu wa sasa, akiwa na clean sheets 11 ndani ya Premier League na kuisaidia klabu yake kushika nafasi ya nane kwenye msimamo wa PL.

Pamoja na Henderson, Sheffield United wamewaongeza mikataba mabeki, Phil Jagielka na Kieron Freeman na kiungo, Jack Rodwell na mshambuliaji, Leon Clarke kwa kipindi chote cha msimu huu. Lakini kiungo Mo Besic amerejea Everton na beki, Panos Retsos amerejea Bayer Leverkusen baada ya mikopo yao kumarizika.

46 MAONI

 1. Henderson yuko vzr kwenye msimu huu ni kuvuta muda tuu ili kuangalia baada ya msimu kama ole atamuweka kwenye mipango yake ya baadae

 2. Ingefaa Man U wakamurejesha Henderson kucheza sambamba na De Gea ambapo atakuwa mrithi sahihi baada ya De Gea kuondoka#meridianbettz

 3. Ni habar njema sana kwan Sheffield United na Manchester United wanatajwa kuwa kwenye mazungumzo ya kumuongezea mkataba Dean Henderson kwa dili la mkopo hadi msimu ujao.
  Golikipa huyu ameweza kufanya vyema akiwa kikosi cha Chris Wilder katika michuano ya Championship na pia kwenye msimu wa ligi
  Kwa mujibu wa ripoti ni kuwa meneja wa Manchester United Ole Gunnar anamuona Henderson kama golikipa wake namba moja kwa siku zijazo, lakini kwa sasa De Gea ataendelea kuwa chaguo ka kwanza la United kwa sasa.
  Wilder amenukuliwa akithibitisha kuwa kuna matumaini ya kumbakiza golikipa huyu kwa angalau mwaka mmoja, na mazungumzo ya kukamilisha hilo yanaendelea na klabu ya Man United
  Lakin tunaona kuwa Henderson atafanya maajabu makubwa akiwa shuffled kuliko akirud man u kwani atakuwa bench hivyo n habari njema sana 👍

 4. Golikipa huyu ameweza kufanya vyema akiwa kikosi cha Chris Wilder katika michuano ya Championship na pia kwenye msimu wa ligi ingekuwa vizuri sana kama Manchester united wangemchukuwa

 5. Maoni:Maamuzi yake ya kuendelea na mkataba wake huko sheffield united yanaeshimiwa ingwawa man u wanamuhitaj.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa