Nyota wa Juventus, Gonzalo Higuain amezungumzia uwezekano wa kwenda Major League Soccer -MLS ya Marekani kama ikiwa ataondoka Juventus.

Juventus sasa ipo chini ya meneja mpya katika maandalizi ya msimu mpya baada ya kutimuliwa kwa Maurizio Sarri. Inaaminika kuwa bika shaka meneja mpya Andrea Pirlo naye atakuja na namna na mfumo wake mwenyewe wa kufanya mambo.

Higuain alitimba Juventus baada ya kufika kwa meneja wake wa Zamani wa Napoli -Maurizio Sarri, lakini hakuweza ku

Higuain anaamini kuwa Pirlo akawa hana mahitaji na baadhi ya wachezaji na hivyo wakalazimika kuondoka klabuni hapo.

Higuain na Mpango wa Kutimba MLS

Higuain, ambaye anafahamu kuwa wachezaji wengi katika umri fulani wanaamua kwenda China, Marekani au Saudi Arabia, anadhani huu unaweza kuwa wakati wake kufikiri juu ya hilo.

Kwa sasa hafikirii kurejea Argentina, na anasema kuwa haja ‘miss’ kucheza soka la Argentina, isipokuwa anapenda tuu kuangalia. Hivyo hii haiwezi kuwa moja ya machaguo yake ikiwa atatakiwa kuondoka Juventus.

“Wengi wanaenda MLS, itakuwa vyema kwangu ndiyo, lakini kwa sasa niko hapa, ngoja tuone nini kitatokea.” -Gonzalo Higuain

Pia anasema kuwa hawezi kuwa kocha kwa sababu ya changamoto na usumbufu na msongo wa mawazo unayoweza kupata kutokana na kazi hii.


 

Drops and Wins!

Umeijua hii? Ni promosheni kabambe ya ushindi kwenye Casino ya mtandaoni ya Meridianbet! Unaweza kushinda hadi Euro 2,000,000 leo.

Soma zaidi ucheze

34 MAONI

  1. MLS imekuwa ligi ya waliokosa nafasi timu za Ulaya. Bado Higuain ana uwezo wa kucheza soka la ushindani Ulaya endapo atapata timu inayomuchezesha mara kwa mara#meridianbettz

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa