Mwenyekiti wa Tottenham Hotspurs, Daniel Levy anaripotiwa kuwa alikuwa na hofu ya wachezaji kadhaa wa kikosi cha kwanza wa Spurs wangelazimika kuondoka klabuni hapo na akalazimika kumtimua Jose Mourinho.

Jumatatu, Spurs walitangaza kuwa wametemana na aliyekuwa meneja wao, wakiwa kwenye maandalizi ya kuumana na Man City kwenye fainali ya Kombe la Ligi.

Mourinho amekuwa meneja wa Spurs kwa miezi 17, akiwaacha Spurs nafasi ya saba nyuma ya West Ham United kwa pointi 5.

Hofu ya Levy Imemtimua Mourinho

Kwa mujibu wa Eurosport, Levy anahitaji kuwabakiza wachezaji kama Harry Kane, Dele Alli na Gareth Bale, na anaamini wangelazimika kuondoka ikiwa Mourinho angesalia klabuni hapo.

Kane amekuwa akihusishwa na kuondoka klabuni hapo, akitajwa kuwavutia Man United na Man City. Dele Alli pia anawavutia PSG, Levy angetamani kuendelea kumbakiza lakini alikuwa amepoteza mvuto kwa Mourinho.

Bale licha ya mkataba wake wa mkopo kuelekea mwishoni, Levy anatarajia kuwa wanaweza kumbakiza. Hivyo, kumtimua meneja Jose ilikuwa ni namna ya kujihami na uwezekano wa wachezaji kadhaa kuondoka klabuni hapo.


 

MKWANJA MARIDHAWA NA KASINO YA 777 MEGA DELUXE

Nafasi nyingine kwaajili yako, kasino mpya yenye hadhi ya kipekee inayokupa kila sababu ya kuwa mshindi katika kasino za Meridianbet, anza siku yako na njia rahisi ya kutengeneza mkwanja.

Mourinho, Hofu ya Levy Imemtimua Mourinho, Meridianbet

CHEZA HAPA

12 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa