Taarifa zaidi zinaibuka juu ya makubaliano ya ufadhili wa Inter Milan na Oaktree Capital, ambaye aliwakopesha Suning €275m, kuwa hatanunua hisa zozote za Inter.

Taarifa iliyotolewa kupitia shirika la habari ANSA ilithibitisha kuwa Suning alikuwa amefanya makubaliano na Oaktree ya ufadhili wa thamani ya €275m, lakini maelezo yalikuwa machache.

Hapo awali, Bloomberg walikuwa wameripoti kuwa Oaktree walilipa €33m kununua asilimia 31 ya umiliki wa klabu kwa Lion Rock na kuwa kama wanahisa wapya wa wa hisa chache, na pia kukopesha €242m ambayo ingetakiwa kulipwa ndani ya miaka mitatu.

Hata hivyo, Il Sole 24 Ore na mwandishi wa Sky Sport Italia Marco Bellinazzo wanasisitiza kuwa hivyo sivyo ilivyo.

Oaktree hawatakuwa wanahisa wa klabu, hivyo Suning atabaki na asilimia 68.5 ya umiliki na Lion Rock zaidi ya asilimia 31.

Fedha zote huenda kwa Great Horizon, kampuni iliyopo Luxemburg inayoshikilia uendeshaji wa Inter.

Inaripotiwa kuwa €35m ya hapo awali itakabidhiwa Inter, halafu zingine zitawasilishwa kwa awamu kadhaa.

Ikiwa Suning watashindwa kufanya malipo ya mkopo, basi Oaktree watachukua hisa zao za umiliki wa klabu.


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

kane, Kane Aweka Wazi Maazimio Yake Kucheza UEFA., MeridianbetBASHIRI SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa