Timu ya taifa ya Italy imekuwa ya kwanza kutinga hatua ya 16 bora katika michuano ya Euro 2020 baada ya hapo jana kushinda magoli matatu dhidi ya Switzerland.

Italy inakuwa imepata ushindi wa pili mfululizo na kujikusanyia alama sita na magoli 6, kitendo kinachowapeleka mpaka nafasi ya kwanza ya kundi A na moja kwa moja mpaka hatua ya 16 bora ikiwa taifa ya kwanza kufanya hivyo.

Magoli mawili ya Locatelli na moja la Immobile yalitosha kuwapa ushindi huo usio wa kutia maji maji wazee wa Italy ambao wamepania sana kubeba kombe hilo licha ya kutopewa uzito sana katika michuano hiyo.

Kwa upande mwigine timu ya Wales ikiwa na Gareth Bale kama nahodha walifanikiwa kupata ushindi wa mabao mawili dhidi ya Turkey ambao wamepoteza mechi zao zote mbili na wala alama 0 na kujishikia nafasi ya mwisho.


SHINDA TSH 150,000,000/=

Mtaani kumechangamka, washkaji wanakamata mkwanja kwa mkakati tu na Footbal Fever! Ni rahisi, changamkia fursa hii kushinda mgao wako wa TSH 150,000,000/= 💰🤑

Atletico, Atletico Waunga Tela kwa Calhanoglu, MeridianbetINGIA MCHEZONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa