Kuelekea dirisha kubwa la usajili barani Ulaya. Jadon Sancho ameanza kuviteka vichwa vya habari kwa mara nyingine msimu huu.

Klabu ya Borussia Dortmund imeripotiwa kupunguza dau la kumsajili nyota wao Jadon Sancho ikilinganishwa na dau lililowekwa msimu uliopita. Itakumbukwa, Man United walielekezwa kulipwa pauni milioni 120 ili kumsajili Sancho msimu uliopita. Hili lilishindikana na Sancho alisalia Signal Iduna Park kwa msimu mmoja.

Vigogo wa EPL – Man United, Liverpool na Chelsea wanatajwa kukaa mkao wa kula na kuingia vitani mapema dirisha la usajili mkubwa litakapofunguliwa mwezi Julai,2021. Baada ya United kumkosa Sancho msimu uliopita, safari hii Liverpool na Chelsea zimejiandaa kuingia ulingoni kuisaka saini ya Sancho kama sehemu ya kujiimarisha kwa msimu ujao.

Mkurugenzi wa michezo wa Dortmund, Michael Zorc alisema “tunamakubaliano na Sancho tangu msimu uliopita. Ataweza kuondoka msimu huu kama vigezo kadhaa vitazingatiwa”


TENGENEZA FAIDA KUPITIA MCHEZO WA TITAN DICE UKIWA NA MERIDIANBET KASINO

Unapokuwa kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, huna sababu ya kucheza kwa mashaka. Titan Dice, ni mchezo unaweza kukupatia mamilioni kwa mzunguko mmoja!

Jadon Sancho, Jadon Sancho Kugonganisha Vigogo EPL., Meridianbet

SOMA ZAIDI

9 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa