James Rodriguez hajawahi kuwa nje ya vichwa vya habari msimu huu wa joto na hatma ya mchezaji huyo wa Everton na mtaifa wa Colombia mpaka sasa haijulikani.
James Rodriguez: Bado Italia Tu Nkamilishe 5.
James Rodriguez wakati akiichezea Monaco ya Ufaransa

Kufuatia kuachwa kwake kwenye kikosi cha Colombia cha Copa America msimu huu wa joto, mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid alisababisha taharuki kwa kumzungumzia kocha Reinaldo Rueda. Sasa, ameuliza maswali juu ya wapi atacheza mpira wake msimu ujao.

“Nimecheza tayari kwenye ligi zote,” James alisema.

“Nimebaki na Italia tu. Itakuwa vizuri kucheza huko na kuwa na rekodi hiyo, lakini sijui kama itatokea siku za usoni.”

James Rodriguez: Bado Italia Tu Nkamilishe 5.
James Rodriguez, Real Madrid

Miamba ya Serie A AC Milan inaripotiwa kuwa na hamu ya kumsajili James msimu huu wa joto na yeye mwenyewe amekiri kuwa hajui atacheza wapi msimu ujao, ingawa amesema kwamba hajioni akirudi Real Madrid.

“Sijui kabisa nitacheza wapi,” James alisema.

“Ni mada ngumu sana. Wacha tuone ni nini kitatokea. Sitaki kusema ndio au hapana kwa sababu sijui nini kitatokea. Ninafanya mazoezi vizuri.

“Kwenye mpira wa miguu haujui nini kitatokea. Ninajua tu kuwa ninafanya mazoezi vizuri na ninafanya kazi kwa bidii, nikifikiria juu ya sasa. Ninafanya mazoezi kwa bidii kwa kile kitakachokuja.”

James Rodriguez: Bado Italia Tu Nkamilishe 5.
Rodriguez, Bayern Munich

KUWA SHUJAA KATIKA KASINO ZA MERIDIANBET!

SHOOT! mchezo unaokupa nafasi ya kupambania ushindi wako mkubwa kwenye kasino ya mtandaoni ya Meridianbet! Usisubiri hii, jiunge sasa kufurahia ushindi!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA SASA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa