Zlatan Ibrahimovic alikuwa mhanga wa kadi pekee nyekundu katika mchezo kati ya Ac Milan na Parma. Milan walifanikiwa kushinda magoli 3-1, huku Ibrahimovic akitoa pasi ya goli moja.

Ibrahimovic alipewa kadi nyekundu kwa hali isiyoeleweka, lakini mwamuzi alidai kwamba Zlatan alimtukana hivyo hakuitaji kupewa kadi ya njano kama onyo.

Kocha wa Mlan alisema alipozungumza na Zlatan alidai kwamba hakumtukana bali alikuwa na majadiliano na mwamuzi kuhusu faulo. Mwamuzi Fabio Mwaresca aliandika katika ripoti yake kuwa Ibrahimovic alimtukana,kitendo ambacho mwamba huyo wa soka anakataa.

Zlatan
Zlatan anapata kadi nyekundu kwa mara nyekundu toka 2018

Ibrahimovic amekuwa akihusika na matukio mbalimbali ambayo yanaelezewa kusababishwa na ujeuri na ubabe wa nguli huyo wa soka. Itakumbukwa mwaka 2018, akiwa na LA Galaxy, Ibrahimovic alipewa adhabu ya kadi nyekundu.

Licha ya kupingwa na watu kwa muda mwingi Zlatan pia huonesha ujuzi wake anapokuwa uwanjani huku akiwa na umri wa miaka 39.

Baada ya ushindi huo wa jana, Ac Milan wamepunguza gap lao na viongozi Inter ambao watakuwa na mechi dhidi ya Cagliari baadaye.

Ac Milan wamesema watakata rufaa kwa kadi hiyo ili kuendelea kumchezesha Ibrahimovic kwenye mechi zilizobaki.


INAWEZEKANA KUWA MILIONEA BILA KUVUJA JASHO NA KASINO YA ODD ONE OUT.

Odd One Out kutoka Meridianbet ni moja ya kasino maridhawa yenye picha halisi, ambayo inakupa nafasi ya kushinda kadri uwezavyo na kuwa milionea mara baada ya mzunguko kukamilika.

Zlatan, Je, Ni Ubabe Au Ujuzi wa Zlatan?, Meridianbet

CHEZA HAPA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa