Italy walitambulisha jezi yao mpya siku moja kabla mchezo wa kirafiki dhidi ya Uruguay. Kumbuka walikuwa wanajiandaa na mechi za kufuzu EURO 2012.

Kesho yake, Italy waliingia uwanjani na jezi zao bila shida. Wakacheza kipindi cha kwanza kikaisha salama, lakini walikuwa nyuma kwa bao moja, isitoshe Balotelli alikosa nafasi mbili za wazi.

Jezi

Waliporejea kipindi cha pili, Balotelli alirudi uwanjani ametinga jezi yake ya zamani, akaonekana tofauti na wengine. Refa alimuonesha kadi ya njano akamuagiza aende kubadilisha.

Alipoenda chumbani kocha wa Italy Cessare Prandelli aliamua kumbadilisha, Balotelli aliporejea akakuta nafasi yake amechukua mchezaji mwingine. Badala ya kukaa benchi, akaondoka zake kurudi chumbani.

Baadae aliulizwa kwanini alifanya vile?? Alijibu kuwa jezi mpya ya Italy ni mbaya sana na haimpendezi. Halafu ubaya wake ndio unasababisha akose magoli😀

Kichaa Super Mario Balotelli ametimiza miaka 31 leo.


SHINDA NA TIKI REWARD KASINO

Unaanzaje siku yako bila kuwa na pesa, Meridianbet kupitia kasino zake za mtandaoni inakupa sababu ya kufanya siku yako kuwa njema. Mchezo maarufu wa Tiki Reward unaweza kukufanya milionea. Cheza sasa kibingwa!

Tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa