Klabu ya Atletico Madrid haitarajii kufanya maamuzi ya kumuuza kiungo wao Joao Felix kwenye dirisha hili la uhamisho.

Juna la Felix limekuwa likitajwa sana kwenye taarifa mbalimbali za masuala ya uhamisho wa wachezaji, baada ya kuwa na msimu wenye panda shuka tangia alipowasili klabuni hapo kwa paundi milioni 127 mwaka 2019.

Kutokana na ada kubwa aliyolipiwa staa huyu amekuwa akikosolewa kwa urahisi zaidi na watu wengi licha ya ukweli kuwa bado anaendelea kujiboresha kama mchezaji.

 Joao Felix
Joao Felix

Joao Felix amefanikiwa kupata magoli 10 na asisti sita wakati Atletico wakifanikiwa kushinda taji la La Liga msimu uliopita.

Atletico wanatarajia staa huyu ataendelea kujiboresha kuwa bora zaidi, na kwa mujibu wa Marca, Felix atakuwa hashikiki kwenye dirisha hili la uhamisho huku klabu ikiwa imepania kumtumia vyema msimu unaokuja.

Hivyo, mpango wa klabu ni kumpa mda wa kuendelea kujiboresha na mpango wa kumuweka sokoni haupo kabisa mezani kwa sasa.


FURAHIA KASINO MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Kasino ya Mayan Eagle inakukufanya kuwa bingwa wakati wowote unapoamua kuicheza. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa