Kila mtu ana maoni yake, yangu ni haya; Dirisha lililopita la usajili, lile kubwa na dogo, Simba walifanya sajili kwa utulivu wa hali ya juu sana. Walitulia na kuangalia mahitaji ya timu, ndiyo maana sura zao mpya zimelipa sana.

Kuanzia kwa Larry Bwalya, Bernard Morrison, Thadeo Lwanga na Chris Mugalu. Sidhani kuna hata mmoja ambaye, Simba wanajuta kumsajili.

Joash

Ukiniuliza mimi, usajili bora zaidi wa Simba katika dirisha lililopita, sitahitaji hata sekunde ya kufikiria, jibu langu litakuwa wazi na lililonyooka, ‘JOASH ONYANGO

Ni beki anayejua maana ya kulinda lango lake. Ni mtu ambaye jina lake unatakiwa ulitaje la kwanza kabisa unapoulizwa mfano wa ‘STOPPER’ mmoja wa uhakika.

Onyango

Joash anakaba sakafuni, anacheza hewani tena uhakika sana. Achana na hilo, Onyango ni mwepesi sana wa kusoma madhaifu ya wenzake hivo anasawazisha makosa yao kwa urahisi mno.

Jina la Chama, show za Bwalya na Miquissone, na magoli ya Mugalu na Kagere, yanafanya baadhi ya kazi za wachezaji wengine zionekane za kawaida, kama inavyotokea kwa Onyango.

Onyango

Nafikiri kati ya wachezaji watatu bora wa msimu wa Simba, jina lake linapaswa kutokea. Joash ni habari nyingine aise. Kwa mabeki wa kati Ligi kuu Tanzania Bara Onyango anatokea dunia yake kabisa.


MKWANJA MARIDHAWA NA KASINO YA 777 MEGA DELUXE

Nafasi nyingine kwaajili yako, kasino mpya yenye hadhi ya kipekee inayokupa kila sababu ya kuwa mshindi katika kasino za Meridianbet, anza siku yako na njia rahisi ya kutengeneza mkwanja.

Joash, Joash Onyango, Simba Hatukudai, Meridianbet

CHEZA HAPA

10 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa