Mchezaji wa Newcastle United, Joe Willock ameweka rekodi ya kuwa mchezaji mdogo zaidi kufunga katika michezo sita ya Premier League kwa mara sita mfulululizo baada ya hapo jana kuisaidia timu yake kushinda goli 1-0.

Willock alifanya hivyo akiwa na miaka 21 na siku 272 tu, katika mechi ambayo ilionekana kuegemea upande mmoja sana ambapo Newcastle United walishambulia lango la Sheffield United kama nyuki waliochokozwa kwenye mzinga wao, alihitajika shujaa mmoja tu kwenda kupakua asali na Joe Willock alifanya hivyo bila hiyana.

Sheffield United ambao tayari wameshuka daraja hawakuonekana kuwa na mipango thabiti lakini vijana wa Newcastle hawakutaka kushuka daraja na walihakikisha wanawapa furaha mashabiki 10000 ambao waliingia uwanjani ikiwa ni jitihada za kurudisha mashabiki uwanjani msimu ujao.

Willock amekuwa mchezaji muhimu kwa Newcastle United hivi karibuni akihusika kwenye magoli 7 ambayo amefunga sita katika michezo sita mfulululizo huku moja akifunga katika michezo ya nyuma. Willock yupo Newcastle United kwa mkopo akitokea Arsenal ambapo hakupata muda mwingi wa kucheza.

Baada ya mchezo wa jana mashabiki wa Newcastle United walionesha hisia zao za kumpenda mchezaji huyo na kumtaka aendelee kusalia klabuni hapo kutoka na mchango mkubwa anaotoa katika klabu yake licha ya umri wake mdogo.

Matokeo hayo ya jana yameisogeza Newcastle United mpaka nafasi ya 15 ikiwa na alama 42, huku Sheffield United ikiendelea kusalia mwishoni ikiwa na alama zake 20.


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

Willock, Joe Willock Aweka Rekodi, Akiifungia Newcastle 1, MeridianbetBASHIRI SASA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa