Licha ya yota wa Juventus na timu ya taifa ya ureno Christiano Ronaldo kukosa penati kwenye mchezo wa marudiano wa kombe la italia lakini timu hiyo ya Juventus imefanikiwa kutinga hatua ya fainali kwa faida ya goli la ugenini, ambapo kwenye mchezo wa awali walienda sare ya kufungana goli 1-1 wakati mchezo wa hapo jana walipata sare nyingine ya kutofungana.

, Juve na Ac Millan Nusu Fainali iliyo Akisi Picha ya Fainali, Meridianbet

Kwenye mchezo wa awali Juventus walianza kupata goli kunako dakika ya 13 ya mchezo baada ya kupata penati ambayo ilipigwa na Christiano Ronaldo, lakini baadae Ac milan walipata bao la kusawazisha hivyo kufanaya dakika tisini zimalizike kwa kutunishiana misuli kwa kutoka 1-1.

Kwenye mchezo huo wa marudiano AC milan iliwakosa nyota wake kama  Zlatan Ibramovic kufuatia kuwa na majeraha huku Samu Castillejo na Theo Hernandez waliukosa mchezo huo

Mechi ya marudiano ilipigwa siku ya ijumaa juni 13 walienda sare nyingine ya kutofungana goli hivyo Juventus kufanikiwa kwenda hatua ya fainali kwa faida ya goli la ugenini, na kuwa fanya Juventus kuongeza rekodi ya kutinga fainali kwa mara ya 19, huku timu ya As Roma kuwa ni ya pili kwa rekodi hiyo kwa kufika fainali ya kombe hilo la Italia  mara 16

, Juve na Ac Millan Nusu Fainali iliyo Akisi Picha ya Fainali, Meridianbet

Fainali ya kombe la italia itafanyika tarehe 17 juni ikiwakutanisha kati mshindi atakae patikana kati ya Napoli dhidi  Inter milan  na timu ya  Juventus , lakini  pia Juventus siku ya juma tatu watacheza   mechi yao dhidi ya Bologna wakiwa ugenini kwenye ligi ya serie A

Siku ya mchezo huo Juventus na Ac milan heshima zao kwa wafanyakazi wote waliojiweka mstari wa mbele kukabaliana na maambukizi ya virusi vya korona  na wote waliopoteza maisha tangu  kuzuka kwa virusi hivyo hatari

39 MAONI

  1. Miaka ya karibuni AC Milan sio ile ya akina Ronaldo De Lima , Gattuso na wengineo. Wamechoka hawana uwezo kuingia sokoni na kutafuta wachezaji wa watakaorejesha heshima iliyopotea. Hata hivyo walijitahidi#meridianbettz

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa