Timu ya Juventus imekanusha uzushi ulionenea hivi karibuni kuhusiana na rais wao Andrea Agnelli kujiuzulu kutokana na Super League.

Hivi karibuni kulikuwa na uzushi kuwa rais huyo wa Juventus amejiuzulu kutokana na timu yake kukataa kujiunga kwenye European Super League ambaye inaonekana kuelekea ukingoni.

Taarifa rasmi kutoka akaunti ya Twitter ya Juventus iliindika kuwa “tunakataa kuhusu kujiuzulu kwa Agnelli”. Taarifa hiyo inaonesha kwamba Juventus inaendelea kuwa Agnelli kama raisi wao.

Agnelli alieleza chombo kimoja cha habari kwamba Europea Super League haitoweza kuendelea kutokana na kujitoa kwa timu kubwa sita za ligi ya Uingereza.

Hapo jana vilabu sita vyote vya EPL, yaani Arsenal, Man United, Man City, Tottenham, Liverpool na Chelsea vilitangaza kujiondoa kwenye mashindano hayo ya Super League. Uamuzi huo umekuja kutokana na mashinikazo mbalimbali kutoka kwa mashabiki wa timu husika pamoja na UEFA na FIFA.

Kufuatia kujitoa kwa Manchester United, inasemekana makamu wa rais wa timu hiyo, Ed Woodward amejiuzulu nafasi hiyo klabuni hapo. Juzi tu Woodward alijitoa kwenye majukumu yake yote ya UEFA na kusababisha Man United kujitoa kwenye umoja wa kabu za ulaya ECA.

Hakika European Super League imekuja na mengi na kuondoka na mengi mno.


MKWANJA MARIDHAWA NA KASINO YA 777 MEGA DELUXE

Nafasi nyingine kwaajili yako, kasino mpya yenye hadhi ya kipekee inayokupa kila sababu ya kuwa mshindi katika kasino za Meridianbet, anza siku yako na njia rahisi ya kutengeneza mkwanja.

agnelli, Juventus: Agnelli Bado Yupo 100%, Meridianbet

CHEZA HAPA

12 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa