Kocha wa Juventus Andrea Pirlo amethibitisha kuendelea kuwa meneja wa Juventus baada ya ushindi wa Copa Italia dhidi ya Atalanta, laikini Ripoti zinasema Juventus wao watafanya maamuzi Jumatatu.

Kwa mujibu wa Tuttosport, Juventus baado wanaendelea kufikiria ikiwa wanaweza kumuongezea muda Pirlo kwa msimu mwingine, lakini hatma yake klabuni hapo bado imetanda giza.

Msimu huu umekuwa mgumu sana kwa Juve, na sasa wanapambania nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa.

Juventus: Pirlo Akanusha Kuchelewesha Mishahara

Vijana wa Pirlo wanahitaji kushinda kwenye mechi wanayosafiri dhidi ya Bologna Jumapili, na pia wanahitaji msaada kutoka kwa Verona au Atalanta, ambao wanakutana na Napoli na Milan, kwa mlolongo huo.

Hata hivyo, sio kwamba kuna ukosefu wa nani anaweza kuirithi nafasi ya Pirlo Juve, ripoti nchini Italia zimekuwa zikiwataja Gennaro Gattuso, Zinedine Zidane, Max Allegri na Simone Inzaghi kama miungoni wa wanaotupiwa jicho kwa kibarua hicho.

Baada ya ushindi huu Pirlo amesisitiza kuwa anataka kuendelea, lakini suala la kufuzu ligi ya mabingwa linaweza kuwa na nafasi kubwa sana katika kuamua hatma yake klabuni hapo.


 

UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

Juventus, Juventus:  Hatma ya Andrea Pirlo Kuamuliwa Jumatatu, MeridianbetBASHIRI SASA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa