Wakala wa Paulo Dybala, Jorge Antun anadaiwa kuwa anatarajia kurejea Argentina baada ya mazungumzo ya mkataba wa mteja wake kusimama.

Mkataba wa sasa wa Paulo Dybala unadumu hadi Juni 2022, lakini nyota huyu amekuwa akisistiza nia yake ya kutaka kusaini kuongeza mkataba wake kuendelea kusalia Juventus.

Wakala wa mchezaji huyu, Jorge Antun analiwasili Italia mwezi uliopita, lakini alishindwa kuonana na raisi Fabio Paratici, kutokana na kutokuwepo na mazingira rafiki kwa mkutano wao kufuatia kutpatikana kwa visa vya Corona klabuni hapo.

Dybala

Kwa mujibu wa chapisho la Tuttorsport, wakala wa staa huyu sasa anatarajia kurejea Argentina bila kuonana na raisi.

Dybala anatarajia kuongezeka dau kwenye mshahara wake wake wa sasa wa euro milioni saba, ambao anatarajia huenda ikawa karibu mara mbili yake kwenye mkataba mpya.

Hata hivyo klabu inaripotiwa kuwa na kigugumizi kufikia dau ambalo analitaka Dybala kwenye mkataba mpya, kwa kile kinachotajwa kuwa ni changamoto ya kiuchumi iliyosababishwa na Corona.


 

TSH.160,000,000 KUSHINDANIWA!

Tunazungumzia mkwanja wa Tshs.160,000,000! Kupitia Kasino ya Mtandaonii ya Meridianbet unaweza kuwa milionea wakati wowote.

Dybala, Juventus: Mazungumzo ya Mkataba wa Dybala Yakwama, MeridianbetKamata Mkwanja wako HAPA

22 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa