Klabu ya Juventus inatarajiwa kuwa itawacheleshea mishahara wachezaji katika jitihada za kuweka sawa vitabu vyao vya fedha.

Kwa mujibu wa chapisho la Corriere dello Sport, Juventus wamewaomba wachezaji wao wakubali malipo ya kuchelewa kwa miezi takribani minne.

Mbinu hii ni jitihada za kuhakikisha masuala yao ya fedha yanakuwa vyema, na ni mbinu ambayo ilitumika awali wakati janga la Corona, lilipoharibu hali ya kifedha katika vilabu vingi vya Ulaya.

Taarifa zinasema kuwa wachezaji wa Juventus walikubali mishahara yao ya miezi ya Machi, Aprili, Mei na Juni 2020 kuchelewesha, na badala yake ililipwa kwenye mwaka wa fedha wa 2020-21.

Hivyo, inaonekana kuwa Juventus wanahitaji kutumia mbinu hiyo hiyo ya kuwaomba wachezaji wakubali kulipwa mishahara yao kwenye mwaka wa fedha wa 2021-22.

Hata hivyo, bado haijafahamika kama wachezaji tayari wameshakubaliana na suala hilo, na ukifuatia miungoni mwao wengine wanaingia kwenye soko la uhamisho la msimu wa joto na hivyo hawana uhakika na hatma yao pale Turin.


 

UNAWEZAJE KUKOSA KASINO YA BREAK AWAY LUCKY WILDS INAYOKUPA NAFASI YA USHINDI MURUA.

Break Away Lucky Wilds ni moja ya Sloti pendwa katika kasino za #meridianbet inayokupa mara 11,000X ya dau lako, unayo nafasi ya kuwa milionea unasubiri nini?

Juventus, Juventus Waomba Kuchelewesha Mishahara, Meridianbet

CHEZA HAPA

4 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa