Timu ya Kaizer Chiefs imeonyesha kuwa wapo makini na mchezo wa marudiano dhidi ya Simba baada ya kuamua kuchukua hoteli pembeni ya mjini huku wakiweka ulinzi mkali.

Timu hiyo kutoka Afrika Kusini iliwasili juzi Mei 20, 2021 na moja kwa moja walienda katika hoteli ya Ramada iliyopo Mbezi Beach.

Kaizer chief vs simbaUlinzi uliopo hapo katika hoteli usipime, mtu anayeingia wanatoka watu wa Kaizer na kuzungumza nae kisha unageuka na kuondoka.

Inaelezwa mabosi wa Kaizer Chiefs wameichukua hoteli hiyo nzima mpaka watakapoondoka kesho baada ya mechi yao dhidi ya Simba.
Kaizer chief ramadaPia Kaizer inaelezwa jana baada ya kuwasili walikataa gari lilioandaliwa na Simba kisha wakaingia katika gari waliloandaa wao kutoka kampuni ya Shabiby.

Awali timu ziizocheza na Simba zilikuwa zinafikia Hoteli ziiizopo mjini, lakini imekuwa tofauti kwa Kaizer Chiefs ambao wapo mbali na uwanja wa mchezo (Benjamin Mkapa).


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

kane, Kane Aweka Wazi Maazimio Yake Kucheza UEFA., MeridianbetBASHIRI SASA

3 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa