Kaizer Chiefs, au the Amakhos wana ushindi wa magoli manne walijipatia katika hatua ya mkondo wa kwanza dhidi ya Simba kule Afrika ya Kusini.

Zikiwa zimesalia saa chache kabla ya mchezo wa marudiano kati ya Simba na Kaizer Chiefs katika mechi ya robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika, afisa masoko wa timu ya Kaizer Chiefs, Jessica Motaung, ameeleza kuwa kikosi chake kimepima Corona mara mbili na majibu yapo sawa hivyo hawategemei majibu tofauti.

Afisa huyo wa masoko anadai kuwa amesikia klabu ya Simba imekuwa ikihusisha na kutumia Corona kama chanzo cha kufunga timu za ugenini na wao wanaonya na kukemea kitendo hicho.

Baada ya kuwasili hapo jana timu ya Kaizer Chiefs jana, walikataa kutumia gari waliloandaliwa na wenyeji wao na kuamua kukodisha gari lingine ikiwa ni jitihada za kuepuka kile kinachodaiwa kuwa ni figisu za Simba.

Mechi hii itapigwa hapo kesho majira ya saa 10 jioni, na Simba italazimika kushinda magoli 5 ili iweze kufuzu kuelekea hatua ya nusu fainali.


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

kane, Kane Aweka Wazi Maazimio Yake Kucheza UEFA., MeridianbetBASHIRI SASA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa