Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur Harry Kane ameripotiwa kuwa na nia ya kuhamia Manchester City msimu huu wa joto.

Baada ya Spurs kumaliza msimu bila taji kwa mwaka wa 13 mfululizo, nyota huyu anaripotiwa kumfahamisha Daniel Levy juu ya nia yake ya kuondoka klabuni hapo msimu huu wa joto.

Nahodha huyu wa Uingereza anaamini kwamba makubaliano yao yangemruhusu kuondoka, lakini Spurs itahitaji pesa nyingi kuidhinisha kuondoka kwake.

Kane Anaitaka Man City

Manchester City inatambulika kuhusishwa na mpango wa uhamisho wa Harry wakati Sergio Aguero akijiandaa kuondoka, na The Mirror wanaripoti kwamba Etihad ndio Kane anapohitaji kuwepo.

Ripoti hiyo inaongeza kuwa mabingwa wa Ligi ya Premia wamefanya mawasiliano juu ya uwezekano wa kumpata staa huyu, ambaye anaweza kutarajia nyongeza ya mshahara wa pauni laki mbili -kwa wiki anaopata Spurs sasa.

Manchester United, Chelsea na Barcelona zote zimetajwa kuwa kumuhitaji mshambuliaji huyo, ingawa meneja Ryan Mason amedhibitisha kuwa hana ufahamu wa nyota huyo wa miaka 27 kuwasilisha ombi la uhamisho.

Akiwa na mabao 22 katika michezo 33 ya Ligi Kuu msimu huu, Kane anachuana na Mohamed Salah wa Liverpool kuwania Kiatu cha Dhahabu.


 

UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

Kane, Kane Anaitaka Man City Msimu Ujao!, MeridianbetBASHIRI SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa