Mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane ameweka wazi matamanio yake ya kucheza mpira wa miguu wa Ligi ya Mabingwa amedhibitisha anataka kuondoka Spurs katika mahojiano na Gary Neville.

 

kane, Kane Aweka Wazi Maazimio Yake Kucheza UEFA., Meridianbet

“Nadhani kuna mazungumzo yatakayofanyika. Ni wakati ambapo lazima nitafakari na kuwa na mazungumzo na mwenyekiti Daniel Levy. Natumai tuna uhusiano mzuri wa kutosha. Baada ya miaka 16, natumai kuwa tunaweza kuwa na mazungumzo ya kweli ”. alianza Kane

 

“Sijui, namaanisha yeye [Daniel Levy] anaweza kutaka kuniuza. Anaweza kuwa anafikiria ‘Ikiwa ningeweza kupata pauni milioni 100 kwa ajili yako, basi kwanini?’ … unajua ninachomaanisha? Sitakuwa na thamani hiyo kwa miaka miwili au mitatu ijayo ”.

 

“Nataka kucheza Ligi ya Mabingwa … sina hamu ya kufanya chochote. Ninataka kucheza kwenye mashindano makubwa zaidi. Siwezi kusema kwamba nitakaa Spurs kwa muda wote lakini pia siwezi kusema kwamba nitaondoka Tottenham ”. aliongeza mchezaji huyo.

Kane atakuwa na mkutano wa moja kwa moja na Tottenham hivi karibuni kuzungumza juu ya maisha yake ya baadaye, anataka kuondoka, Spurs bado wako kwenye msimamo sawa na vile wanataka kumbakiza. Kane pia atakataa pendekezo jipya la mkataba, kuanzia leo.

Manchester City ndio wanaomuwania zaidi kumsajili Harry Kane msimu huu wa joto, ikiwa Tottenham itakuwa wazi kuzungumza.


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

kane, Kane Aweka Wazi Maazimio Yake Kucheza UEFA., MeridianbetBASHIRI SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa