Mchezaji wa Tottenham Hotspurs, Harry Kane amesema kwamba anatamani kuwa kwenye timu inayochukua mataji mengi.

Kane aliyasema hayo katika mahojiano na chombo kimoja cha habari baada ya timu yake kupoteza mechi ya fainali ya Carabao Cup dhidi ya Manchester City. Bado kumekuwa sintofahamu kuhusiana na hatima ya mchezaji huyo klabuni hapo.

Kane atakumbukwa kuwa na kipindi kizuri msimu uliopita akitengeneza ‘duo’ nzuri na hatari sana na mchezaji mwenzake Son lakini msimu huu mambo si mambo kwani wametolewa kwenye mashindano yote huku wakishika nafasi ya saba katika ligi.

Harry anaeleza kuwa msimu huu ni mgumu na unaovunja moyo sana kwa kuwa hawajafanya vizuri na wanapitia wakati mgumu sana. Kane alikuwa pia miongoni mwa wachezaji wachache walioumizwa kutoka na kufukuzwa kazi kwa kocha wao Jose Mourinho.

Bado haijajulikana kama mchezaji huyo raia wa Uingereza atasalia klabuni hapo au ataondoka lakini kama anatamani kubeba makombe mengi basi bila shaka atalazimika kwenda timu kubwa yenye malengo makubwa na wala sio kubaki hapa Spurs!


KWANI MERIDIANBET WANASEMAJE! MKWANJA UPO KWENYE KASINO MPYA YA MINI POWER ROULETTE.

Unawezaje kukosa ubingwa ndani ya kasino hii maridhawa, Nafasi ya kushinda mkwanja ni kwa kila mtu, Meridianbet inakupa nafasi ya kuwa mmoja ya washidi leo, unasubiri nini?

Mini Power Roullete

CHEZA HAPA

 

17 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa