Mchezaji wa Chelsea N’golo Kante alikuwa na mchezo mzuri sana katika mechi ya mkondo wa kwanza wa nusu fainaliya Champions League dhidi ya Real Madrid pale Estadio De Stefano.

Kante alicheza vizuri sana eneo la katikati ya uwanja akikaba ipasavyo na kuwazuia viungo wa Madrid Kroos, Casemiro na Modric kutawala eneo hilo. N’golo alifanikiwa kushinda mipira mingi ya juu na kutuliza na kupandisha mashambulizi juu.

Baada ya mechi hiyo Kante alipata tuzo ya mchezaji bora wa mechi hiyo. Mchezaji wa zamani wa Chelsea Cesc Fabregas akasema kwamba mchezaji huyo ni mchezaji wa mechi kubwa na huwezi kumshuku anapokuwa uwanjani.

kante
Kante akishindana ubavu na Casemiro katikati ya dimba

Chelsea wametoka na sare ya 1-1, magoli ya Pulisic wa Chelsea na Karim Benzema wa Madrid yakaamua mchezo huo. Chelsea wana nafasi nzuri ya kufuzu fainali endapo watashinda hata goli 1-0 pale Stamford Bridge baadae mwezi huu.

Katika mechi hiyo Madrid ilimkosa nahodha wake Sergio Ramos ambaye alikuwa nje kwa majeruhi, kama mchezaji huyo atakuwa poa katika mechi ya marudiano basi uwezekano wa Madrid kutoruhusu bao utakuwa mkubwa!


KWANI MERIDIANBET WANASEMAJE! MKWANJA UPO KWENYE KASINO MPYA YA MINI POWER ROULETTE.

Unawezaje kukosa ubingwa ndani ya kasino hii maridhawa, Nafasi ya kushinda mkwanja ni kwa kila mtu, Meridianbet inakupa nafasi ya kuwa mmoja ya washidi leo, unasubiri nini?

Mini Power Roullete

CHEZA HAPA

11 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa