Beki wa kulia wa Timu ya Simba Sc, Shomari Kapombe ameongeza mkataba wa kuendelea kusalia klabuni hapo baada ya tetesi kuwa anaweza kutimka klabuni hapo kutokana na mkataba wake kuelekea ukingoni!

Kapombe amekuwa ni mchezaji wa tatu mzawa kusaini mkataba wa kuendelea klabuni hapo, baada ya John Bocco na Mohamed Hussein Kufanya hivyo hapo jana.

Wachezaji wa Tanzania wamekuwa wakitajwa kuwa na thamani ya chini ukitofautisha na wale wa Nje lakini wadau wengi wa soka wanaamini klabu ya Simba imefanikiwa kuwapa jeuri na heshima ya kipekee wachezaji hao wazawa.

Simba inaendela kujipanga na klabu bingwa Afrika na pengine ndio sababu ya kuhakikisha wanaendelea kusalia na wachezaji wao bora akiwemo Kapombe ili kuwa na kikosi chenye muunganiko mzuri kwa muda mrefu lengo likiwa ni kuwa mabingwa wa Afrika.

Ikiwa inaendelea kusubiri timu itakayopangwa kwenye hatua ya robo fainali ambao droo yake itafanyika leo majira ya saa tisa alasiri, Simba inajiandaa na mchezo wa Shirikisho la Azam dhidi ya Kagera Sugar mchezo utakaochezwa kesho saa moja usiku pale kwa Mkapa!


KWANI MERIDIANBET WANASEMAJE! MKWANJA UPO KWENYE KASINO MPYA YA MINI POWER ROULETTE.

Unawezaje kukosa ubingwa ndani ya kasino hii maridhawa, Nafasi ya kushinda mkwanja ni kwa kila mtu, Meridianbet inakupa nafasi ya kuwa mmoja ya washidi leo, unasubiri nini?

Mini Power Roullete

CHEZA HAPA

13 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa