Siku, Masaa, Dakika na Sekunde hufanya kubadilika Kwa majira na namba za Miaka. Mwaka 2015 miaka 6 iliyopitia ilikuwa ni mara ya mwisho kuiona jezi nambari 10 ya timu ya Taifa ya Ufaransa ikiwa mbele, mgongoni Kwa Shekhe Karim Benzema.

Mwaka 2016 ikiwa ni kambi ya maandalizi ya Michuano ya Euro Karim aliondolewa Kambini na Mwalimu Didier Deschamps na kujikuta akikosa michuano yake ya tatu ya Euro baada ya Ile ya Kwanza ya 2008 akiwa kinda pamoja na 2012.

Mambo ya nje ya uwanja, yalimgharimu Benzema. Utovu wa nidhamu na kufanya mambo kinyume na maadili ya mwanadamu. Benzema alidaiwa kusambaza picha za ngono za mchezaji mwenzake Kwa Wakati huo Mathieu Valbuena.

karim

Waziri Mkuu wa Ufaransa Kwa Wakati huo Maneu Valls alisema Benzema hana nafasi tena kwenye timu ya Taifa ya Ufaransa Kwa jambo hili” kutokana na kauli hiyo Mwalimu Deschamps alimuacha.

Licha ya kuwa na takwimu nzuri ndani ya timu hiyo, bado maisha yake yamekuwa magumu Kwa miaka 6. Katika miaka 8 aliyotumikia Ufaransa na kuikosa Kwa miaka 6, Benzema amecheza michezo 81 na kufunga magoli 27.

Safari ya basi huisha mwisho wa kituo wa kituo chake wengine ni washukia njiani Tu! Mara kadhaa Benzema alionyesha matamanio yake ya kurudi kuchezea Taifa lake Asili la Algeria aliitamani michuano ya AFCON. Alikuwepo pale Cairo kushuhudia nduguze wa damu Algeria wakitwaa ubingwa wa AFCON.

karim, Karim Benzema na Ufaransa ni Nyumbani, Meridianbet

Ikiwa mawazo yake yanazidi kuiwaza Africa na AFCON yake, wanaharakati na Wachambuzi wa michezo mara nyingi Walishauri kuona Deschamps akimrejesha kikosini. Kipindi cha miaka 6 nje ya timu ya Taifa, Karim amekuwa Moto kweli kweli akiwa na Real Madrid, amefunga magoli 141 tangu 2015 tu.

Ametwaa mataji makubwa yote ngazi ya Klabu Kwa Kipindi hicho cha miaka 6 ya nje ya timu ya Taifa, Laliga mara 2, UEFA Champions league 3, ikifanya jumla awe na zaidi ya mataji 10 ndani ya misimu hiyo 6.

karim, Karim Benzema na Ufaransa ni Nyumbani, Meridianbet

Karim Benzema Kwa mara ya kwanza amerejea timu ya Taifa. Ni yule yule Mwalimu aliyemuacha mwaka 2016 ndiye aliyemuita sasa, Didie Deschamps, Jana amemwita kikosi Kareem Benzema. “Tumefanya mazungumzo Kwa Marefu sana hatimaye tumekabaliana”

karim, Karim Benzema na Ufaransa ni Nyumbani, Meridianbet


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

karim, Karim Benzema na Ufaransa ni Nyumbani, MeridianbetBASHIRI SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa