Hayawi hayawi sasa yamekuwa, kiungo fundi wa mpira, raia wa Ubelgiji na klabu ya Manchester City – Kevin De Bruyne [KDB], ameongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo mpaka 2025.

KDB ambaye atatimiza miaka 30 mwezi Juni mwaka huu, amefikia hatua hiyo baada ya kukamilisha mchakato wa majadiliano ya mkataba mpya bila ya kutumia wakala yeyote.

De Bruyne alijiunga na City mwaka 2015 akitokea klabu ya Wolfsburg ya nchini Ujerumani. Tangu atue City, Kevin De Bruyne amebeba mataji 7 na kama City watafanikiwa kubeba mataji 4 msimu huu, basi atakuwa amebeba mataji 11 akiwa na miamba hii ya soka la Uingereza.

Kevin De Bruyne, Kevin De Bruyne, Aongeza Miaka 2 City., Meridianbet
KDB akiteta jambo na Pep Guardiola.

“Ninafurahi sana. Tangu nimejiunga na City (2015), nimekuwa nikijihisi nipo nyumbani. Nawapenda mashabiki, familia yangu imetulia hapa Manchester na uchezaji wangu umeboreka mara dufu.

“Ninacheza mpira bora zaidi kwenye maisha yangu ya soka, kiukweli ninahisi kuna mengi mazuri yanakuja. Mimi na Pep tunautizama mpira kwa namna moja. Kuwa na mahusiano hayo na kocha ni muhimu sana kwangu kwa sababu malengo yetu yanaendana, wote tunataka kitu kimoja” alisema KDB.


INAWEZEKANA KUWA MILIONEA BILA KUVUJA JASHO NA KASINO YA ODD ONE OUT.

Odd One Out kutoka Meridianbet ni moja ya kasino maridhawa yenye picha halisi, ambayo inakupa nafasi ya kushinda kadri uwezavyo na kuwa milionea mara baada ya mzunguko kukamilika.

Kevin De Bruyne, Kevin De Bruyne, Aongeza Miaka 2 City., Meridianbet

CHEZA HAPA

4 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa