Rais wa Barcelona Joan Laporta anaripotiwa kufikiria kumtimua Ronald Koeman baada ya kuwa na msimu mgumu klabuni hapo.

Mholanzi huyo alishinda taji moja la Copa del Rey, lakini Barca ilitolewa hatua ya mtoano dhidi ya Paris Saint-Germain kwenye Ligi ya Mabingwa na wamepokea kichapo cha 2-1 dhidi ya Celta Vigo mwishoni mwa wiki na kupoteza matumaini ya taji la La Liga.

Mkataba wa Koeman huko Camp Nou hautakamilika hadi mwisho wa msimu ujao, na anataka klabu kumuamini kuendelea kushika hatamu hadi 2022.

Kibarua cha Koeman Mashakani

Bosi huyu wa Blaugrana yuko tayari kukutana na rais Laporta mwishoni mwa msimu kujadili hatma yake, lakini Marca wanadai kwamba mkuu wa Barca anafikiria ikiwa atamfuta Koeman kabla ya mwanzo wa msimu ujao.

Hata hivyo, ripoti hiyo inadai kwamba kumwondoa kazini bosi huyo kutazidisha hali mbaya ya kifedha ya Barca, ingawa meneja wa zamani wa Everton na Uholanzi anachukuliwa kuwa ameshindwa kuipa klabu kilichotarajiwa.

Kiungo hwa zamani wa Barcelona, Xavi anafikiriwa kuwa na nafasi nzuri ya kupokea kijiti kutoka kwa Koeman, licha ya kusaini mkataba mpya na mabingwa wa Qatar Al-Sadd wiki iliyopita.


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

Koeman, Kibarua cha Koeman Mashakani, MeridianbetBASHIRI SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa