Mshambuliaji Kibu Denis amebamba sana midomoni mwa wapenda soka baada ya kucheza kwa kiwango cha juu kwenye mchezo wa Kirafiki wa Kimataifa pale Tanzania ilipoumana dhidi ya Malawi.

Kwa wengi wengi, safari ya soka ya Kibu Denis ni kitendawili, kwa kuwa hawajui Kibu Denis ametoka wapi kufika alipo leo, baadhi wamemfahamu baada ya kusajiliwa na Mbeya City.

Wacha tukumegee kidogo, safari ya Kibu imeanzia Kumuyange FC, huko Ngara, Kagere alikokuwa anacheza Ligi Daraja la Tatu, akacheza na kuipandisha Ligi Daraja la Pili. Geita Gold FC ya huko Geita ilimpenda na kuhitaji huduma yake hivyo wakamsajili wakiwa wanacheza Ligi Daraja la Kwanza.

Kibu Denis

Mbeya City walimuona kwenye mechi za Play Offs msimu uliopita. Mbeya City wakati huo wakipambania kutoshuka daraja huku Geita Gold FC wenyewe wakipigana kupanda Ligi Kuu.

Mbeya City walifanikiwa kubaki Ligi Kuu baada ya kushinda kwa matokeo ya jumla. Safari ya soka ya Kibu Denis ikaendelea baada ya kusajiliwa na Mbeya City. Kibu Denis  alishiriki kwa mara ya kwanza kwa kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akiwa Mbeya City huku akicheza kwa mara ya kwanza Ligi Kuu, timu yake haifanyi vizuri kwenye ligi, kwa sasa inapambana isishuke daraja lakini Kibu Denis anawasha moto si mchezo hadi kocha wa Taifa Stars Kim Polsen akamwita Stars.

Hii imekuwa mara ya kwanza kwa Kibu kuitwaa kwenye kikosi cha timu ya Taifa, lakini pia alipata fursa ya kucheza kwa mara ya kwanza akiwa amevaa jezi ya timu ya Taifa kwenye gemu hiiya Tanzania dhidi ya Malawi.


 

SHINDA TSH 150,000,000/=

Mtaani kumechangamka, washkaji wanakamata mkwanja kwa mkakati tu na Footbal Fever! Ni rahisi, changamkia fursa hii kushinda mgao wako wa TSH 150,000,000/= 💰🤑

Atletico, Atletico Waunga Tela kwa Calhanoglu, MeridianbetINGIA MCHEZONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa