Wakati tukio alilofanya Christiano Ronaldo kipindi cha mechi kati ya Ureno na Serbia likionesha kuchukiza watu wengi duniani licha ya ukweli kwamba alikuwa sahihi, kitambaa cha unahodha kilichotupwa nyota huyo kimetumika kukusanya Euro 64000 kwa ajili ya matibabu ya kijana wa kiserbia mwenye matatizo wa mgongo.

Wakati wa mechi ya mzunguko wa pili wa michuano ya kufuzu kombe la dunia 2022 kati ya Ureno na Serbia, dakika za mwisho Ronaldo alifunga goli lingeipa ushindi Ureno wa 3-2 lakini mwamuzi wa mchezo alikataa. Kitendo ambacho kilisababisha Ronaldo kutoka nje ya uwanja na kutupa kitambaa cha unahodha chini.

kitambaa cha unahodha cha ronaldo
Mfanyakazi wa zimamoto akiwa na kitambaa hicho

Baada ya Ronaldo kufanya hivyo watu wengi walionekana kupingana vikubwa na kitendo cha nguli huyo wa soka duniani, wakidai kwamba ameshindwa kuonesha uzalendo kwa timu yake ya taifa. 

Marejeo ya picha ya tukio hilo sehemu mbalimbali yalionesha kuwa mpira huo ulipita mstari na lilikuwa ni goli halali. Mwamuzi wa mchezo huo aliomba radhi kutokana na tukio hilo lakini haikuwa na faida yoyote kwa Ureno.

Kitambaa cha Unahodha alichotupa Ronaldo kiliokotwa na kugeuzwa kama chanzo cha kukusanya mapato kwa ajili ya kumsaidia mtoto mwenye matatizo ya mgongo. Kwa sasa Ronaldo anaweza kuwa na amani kwani kitendo chake kimetumika kwa ajili ya jambo chanya na la kibinadamu kwa mwenye uhitaji!

UNAWEZAJE KUKOSA KASINO YA BREAK AWAY LUCKY WILDS INAYOKUPA NAFASI YA USHINDI MURUA.

Break Away Lucky Wilds ni moja ya Sloti pendwa katika kasino za #meridianbet inayokupa mara 11,000X ya dau lako, unayo nafasi ya kuwa milionea unasubiri nini?

kitambaa, Kitambaa Cha Unahodha Cha Ronaldo Chakusanya Euro 64000!, Meridianbet

CHEZA HAPA

5 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa