Leo klabu ya Genoa wanasherekea kutimiza miaka 125, Klabu hii ilianzishwa Septemba 7, 1893 ikiwa kama kama timu ya Kriketi na Wakimbiaji, kwa wakati huo upande wa soka ulikuwa ni mpango unaofuata.

Mwaka 1897, James Richardson Spensley alianzisha upande wa soka wa klabu ya Genoa ikiwa kama moja ya klabu chache sana za mpira wa miguu kwa wakati huo nchini Italia huku nyingi zikitokea Torino. mfano Torino Football & Cricket Club, Nobili Torino na  Internazionale Torino zote zilikuwa ni washindani wa Genoa.

Timu hizo, pamoja na Genoa zilicheza kwenye kinyang’anyiro cha taji la Ngao kwa siku moja na Genoa wakashinda. Mafanikio ya Ginoa yalikuja kupatikana zaidi baada ya vita ya kwanza ya dunia kabla hata ya kuwepo wa Serie A.

Licha ya kutokuwa na mataji mengi katika kutimiza miaka 125, Klabu hii inabaki kuwa moja kati ya klabu zenye historia ya aina yake na kongwe zaidi nchini Italia ambazo bado zinaishi, kwa upande wa timu ya soka umri wake unapishana kidogo kwa miezi kadhaa na Klabu ya Juventus ambayo ilianzishwa Novemba 1, 1897.

Genao wanaripotiwa kuwa, licha ya kushinda ligi nyingi kabla ya uwepo Serie A, bado ushindi wao ubingwa wao wa mara 9 nje ya serie A upo kwenye rekodi wakiwa wanashika nafasi ya 4 kwenye klabu zenye mafanikio kwa kuangalia mataji mbele ya Roma, Lazio, Napoli na Torino, Happy birthday Genoa!

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa