Baada ya kocha wa Chelsea Frank Lampard kudai kwanba Liverpool wana kiburi, Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amemuambia ajifunze kuficha hisia zake baada ya mchezo kumalizika.

Klopp amesema Lampard alivuka mpaka kudai kwamba wao wana kiburi baada ya kutwaa ubingwa wa ligi msimu huu. Klopp amesema anaweza kuvumilia neno lolote wakati mchezo unaendelea, ila baada ya mchezo, haifai kuendelea kulaumu.

Klopp - Bwana Mdogo Tulia, Klopp – Bwana Mdogo Tulia, Meridianbet

Akizungumza kwenye Televisheni baada ya kichapo cha 5-3 kutoka kwa Liverpool, Lampard alisema “Liverpool wajaribu kuacha kiburi kutokana na mafanikio waliyoyapata.” Hayo yalikuja baada ya Klopp kutupiana maneno na Lampard wakati mchezo unaendelea baada ya Kovacic kuvaana na Sadio Mane.

Klopp - Bwana Mdogo Tulia, Klopp – Bwana Mdogo Tulia, Meridianbet

Jana akizungumza Klopp alisema “Hatuna kiburi, na Lampard alikuja kiushindani sana. Namuheshimu kwa hilo. Ila hakupaswa kuendelea kuongea baada ya mchezo. Mambo yote yanatakiwa yaishe filimbi ya mwisho inapopigwa.”

Klopp - Bwana Mdogo Tulia, Klopp – Bwana Mdogo Tulia, Meridianbet

“Alikuja hapa kushinda au kutafuta alama moja ili aipeleke Chelsea UEFA msimu ujao. Bado ni meneja mdogo. Anatakiwa ajifunze kumaliza mchezo ndani ya uwanja. Nisiongelea hili kama angenyamaza baada ya mchezo kumalizika.”


Kwa sababu ya thamani ya pesa yako, kwa kila muamala unaofanya wa kuweka pesa kwenye akaunti yako ya Meridianbet unapata 5% bonasi.

Soma Zaidi

39 MAONI

  1. Lampard achana na mneno maneno ambayo hayawezi kukupa wewe manufaa yoyote kwenye mpira muache klopp anayejua anajua tuu hata ukimtupia maneno gani na ndio maana wewe ukiendeleza kuimba taarabu yeye anapata ubingwa

  2. Ha ha ha yani klopp anajiona sasa bigwa wa miaka yote kwa kutba kuko asijisahau kama wahenga wanasema aliye kuwa juu msubiri chini alafu mawe utatamba mwaka ni wenu Liverpool kuonyesha ujeuri ila Chelsea bado nafasi ipo kama watafanya vizuri kila la heri Chelsea ikiongozwa na kocha Lampard

  3. Lampard alitaka sana kushinda lakini bahati haikuwa upande wake na hilo linatia hasira kidogo mambo yanapokuwa mabaya#meridianbettz

  4. Hii ni kawaida kwa amakocha kutupiana maneno lakini siku ile Chelsea walikuja kizinduka baadae baada ya maafa makubwa, Uchaguzi juu ya first eleven haukuwa mzuri kwa Lampard hivyo Liverpool walichukulia jambo la faida kwao na kuwatandika ipasavyo Chelsea

  5. Klopp yuko sahihi kabisa mwisho wa filimbi ya mwisho ndio mwisho wa maneno maneno mikwaluzano katika mchezo sawa sawa klopp kumuita lampard bwana mdogo ni kweli atulie bwana mdogo lampard ana spirit ile ya ukocha ilibid akae kimya tuu na kuangalia nn afanye au wapi amekosea kuchezea kichapo yeye basi amekua akileta maneno yasiyo faa kama kocha anasema Liverpool wanakibuli hao wachezaj wake watafanya nn lazima ajifunze kukaa kimya ili kutafuta suluhisho alikosea wapi

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa