Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amekiri kwamba nafasi ya kuchukua kiatu cha dhahabu kwa mara ya tatu katika Premier League imemfanya Mohamed Salah kuongeza ubinafsi.

Klopp: Golden Boot Imeongeza Ubinafsi Kwa Salah

Meneja huyo wa The Reds amesema kwamba mshambuliaji huyo wa Misri anaonekana kukitaka kiatu kwa mara nyingine.

Salah alimaliza msimu 2017-18 katika Premier League akiwa na mabao 32 na kushinda zawadi hiyo na mwaka uliyofuatia alimaliza akiwa na mabao 22 ambapo Sadio Mane na Pierre-Emerick Aubameyang pia walimaliza wakiwa na idadi hiyo hivyo wote walitwaa kiatu cha dhabau msimu wa 2018-19.

Klopp: Golden Boot Imeongeza Ubinafsi Kwa Salah
Mohamed Salah, Sadio Mane na Pierre-Emerick Aubameyang wakiwa na Viatu vya Dhahabu baada ya kushinda zawadi hiyo

Msimu huu Salah anashika nafasi ya pili katika chati ya utupiaji mabao amefunga mabao 19 nyuma ya Harry Kane ambaye ana magoli 21 na amesaliwa na michezo 7 pekee kukamilisha msimu.

Klopp alipoulizwa kuelekea mchezo dhidi ya Leeds siku ya Jumatatu kama Kiatu cha Dhahabu ndiyo kipaumbele kwa Salah alijibu: “Ndiyo, ni kweli.

“Wachezaji wengi hawajawahi kushinda kiatu hicho kama ukishinda kwa mara ya kwanza ni mafanikio makubwa, kama ukishinda kwa mara ya pili ni mafaniko makubwa zaidi, kama ukishinda kwa mara ya tatu ni nzuri sababu siyo wachezaji wengi walishinda mara tatu kiatu hicho.

“Straika wanapaswa kuwa wabinafsi , sijawahi kukutana na starika ambaye siyo mbinafsi unaweza kuwa mtu poa lakini mwishoni  unataka kufunga goal.


MKWANJA MARIDHAWA NA KASINO YA 777 MEGA DELUXE

Nafasi nyingine kwaajili yako, kasino mpya yenye hadhi ya kipekee inayokupa kila sababu ya kuwa mshindi katika kasino za Meridianbet, anza siku yako na njia rahisi ya kutengeneza mkwanja.

Klopp, Klopp: Golden Boot Imeongeza Ubinafsi Kwa Salah, Meridianbet

CHEZA HAPA

9 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa