Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp ashangazwa sana na kitengo cha kocha Gareth kumuacha Trent Alexander Arnold nje ya kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kwenye michuano ya kufuzu kombe la dunia 2022. 

Trent mwenye umri wa miaka 22 amekuwa katika moto sana misimu iliyopita akiwa kama beki wa kulia machachari sana. Lakini msimu huu alianza akiwa na maambukizi ya Korona, ila amejitahidi mpaka mwisho kurudi kikosi cha Liverpool.

Katika mahojiano na jarida moja, Klopp alidai kushangazwa sana na kitendo cha kocha wa Uingereza kumuacha Trent Arnold nje ya kikosi. Alisema kama kweli ni muda wao kama makocha wanafanya maamuzi magumu sana ambayo watu wengi hawaelewi. Lakini kumuacha beki bora wa dunia kwa sasa ni maajabu!

Itakumbukwa kuwa Trent amekuwa akijulikana kwa aina ya uchezaji wa beki wa kupanda juu na mara zote krosi zake zimekuwa zikitoa magoli. Moja ya krosi ama pasi ya goli iliyotolewa na Arnold ni wakati wa mechi ya nusu fainali ya marudiano ya ligi ya mabingwa dhidi ya Barcelona ambapo alitoa krosi ya haraka sana na Origi akafunga goli. Nusu fainali ambayo ilikuwa ya kipekee iliyowapeleka Liverpool fainali Kiev kwa Ushindi wa 4-0.

Maamuzi ya kocha Gareth Southgate yamekuwa yakihojiwa sana na huenda pia kikosi hicho kiwakosa Jadon Sacho na Jack Grealish endapo Jesse Lingard ataendelea kufanya Vyema. Trent anaweza akakosa kushiriki michuano ya Euro 2020, endapo Kyle Walker, Kieran Trippier na Reece James wataendeleza makali yao.


UNAWEZAJE KUKOSA KASINO YA BREAK AWAY LUCKY WILDS INAYOKUPA NAFASI YA USHINDI MURUA.

Break Away Lucky Wilds ni moja ya Sloti pendwa katika kasino za #meridianbet inayokupa mara 11,000X ya dau lako, unayo nafasi ya kuwa milionea unasubiri nini?

Trent, Klopp Ashangaa Kuachwa Kwa Trent Uingereza!, Meridianbet

CHEZA HAPA

4 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa