Jurgen Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool amesema kuwa timu hiyo ina jukumu la kuendelea kushinda kila mechi ndani ya Ligi Kuu England ili kuweza kutetea taji lao.

Liverpool ambao ni mabingwa watetezi wa Kombe hilo usiku wa kuamkia leo waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 mbele ya Arsenal inayonolewa na Mikel Arteta kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa Uwanja wa Anfield.

Arsenal ilianza kuwatungua Liverpool dakika ya 25 kupitia kwa Alexandre Lacazette lilidumu kwa muda wa dakika mbili pekee kwani Liverpool waliweka mzani sawa kupitia kwa Sadio Mane dakika ya 28.

Wakati Arsenal inayomtegemea Pierre Emerick Aubameyang kwenye upande wa kutupia mabao ikihaha kutafuta ushindi ilitunguliwa bao la pili dakika ya 34 na Andrew Robertson na dakika ya 88 msumari wa tatu ulipachikwa na Diogo Jota.

Klopp, Klopp – Tutatetea Ubingwa, Meridianbet

Klopp amesema kuwa ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea ikiwa ni pamoja na kushinda tena taji la Ligi Kuu England kazi yao ni moja kuendelea kushinda mechi zao zote.

“Haikuwa rahisi ila nimeona kiwango cha wachezaji ni kizuri wananifurahisha wamefanya vizuri na kazi ni moja tu kutafuta ushindi,” amesema.

Beti kwa Kitochi Kushinda 300,000,000!

Unajua kuwa unaweza kushinda milioni mia tatu kwa buku tu? Ndiyo! Unaweza kushinda kwa kupiga *149*10# na kubashiri. Ingia mchezoni!

Soma Zaidi

34 MAONI

  1. Hanacho kisema Klopp kipo sahii anataka kuja Tena kivingine kuja kuchukua tena taji ataweza tuu navyo muerewa mzee huyo yupo makini natimu yake

  2. Hanacho kisema Klopp kipo sahii anataka kuja Tena kivingine kuja kuchukua tena taji ataweza tuu navyo muerewa mzee huyo yupo makini natimu yake

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa