KUELEKEA kwenye mchezo wao wa ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting, Uongozi wa KMC umeweka wazi viingilio vya mchezo huo ambapo mzunguko itakuwa ni 3000 huku VIP ikiwa ni 5000.

Mchezo huo utapigwa Oktoba 7, mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar ambapo KMC wakiwa na kumbukumbu ya kutoka suluhu katika mchezo uliopita dhidi ya Namungo.

Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa: “Maandalizi ya mchezo wetu dhidi ya Ruvu Shooting yanaendelea vizuri na kikosi kinaendelea na mazoezi chini ya Kocha Mkuu, Hitimana Thierry.

“Morali ya wachezaji ipo juu, viingilio vya kukiona kikosi cha VVIP kwa mzunguko ni 3000 na kwa VIP itakuwa 5000 hii ni maalum kwa mashabiki wetu kuja kukiona kikosi chetu ambacho ni bora sana kwa msimu huu.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa