Afrika Kusini imeondolewa rasmi kwenye mashindano ya kuwania kufuzu AFCON 2022 huko Cameroon, huku ikimuacha kwenye hatari kubwa Kocha mkuu wa timu hiyo. Bafana Bafana walipokea kichapo cha magoli mawili kwa sifuri dhidi ya timu ya taifa ya Sudan huko Khartoum Sudan hapo jana.

Baada ya kushiriki katika mashindano kwa takribani miaka kumi mfululizo mabingwa hao watashindwa kushiriki mwaka 2022. Wapenda soka wa Afrika kusini watakosa mashindano hayo yanajumuisha timu bora za mataifa ya Afrika.

Bafana Bafana
Kocha mkuu wa Bafana Bafana wakati wa mechi dhidi ya Sudan

Bafana Bafana walitakiwa aidha ushindi ama kutoka sare ili kujihakikishia kushiriki AFCON 2022, lakini wakashindwa baada ya Saifedeldin Maki kuifungia goli la kwanza lililofungwa dakika ya tatu na lingine lililofungwa dakika ya 32 kwa timu ya Sudan.

Bafana walijaribu kutafuta goli ambalo lingeweza kuwarudisha mchezoni lakini hawakufanikiwa, waliambulia kupiga mwamba mara kadhaa na jitihada kubwa za kipa wa Sudan.

Kutokana na matokeo hayo, Ntseki pamoja na benchi lake la ufundi atakuwa kwenye wakati mgumu kujibu maswli ya wapenda soka wa Afrika Kusini. Mashabiki wameanza kutoa mawazo yao mtandaoni kwa kutaka Kocha huyo aachwe.


UNAWEZAJE KUKOSA KASINO YA BREAK AWAY LUCKY WILDS INAYOKUPA NAFASI YA USHINDI MURUA.

Break Away Lucky Wilds ni moja ya Sloti pendwa katika kasino za #meridianbet inayokupa mara 11,000X ya dau lako, unayo nafasi ya kuwa milionea unasubiri nini?

bafana bafana, Kocha wa Bafana Bafana Molefi Ntseki Hatihati kupoteza kibarua chake, Meridianbet

CHEZA HAPA

4 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa