Ronald Koeman amefurahishwa na alichokiona kutoka katika kikosi chake cha Barcelona kwenye ushindi wa 3-1 dhidi ya Girona mchezo wa kujipima kabla ya kuanza kwa msimu mpya.
Koeman Ampa 5 Depay Baada ya Mechi ya Kwanza na Barca
Memphis Depay akipiga adhabu ya penati dhidi ya Girona

Mchezo huo uliona Memphis Depay akicheza kwa mara ya kwanza tangu ajiunge na The Blaugrana akitokea klabu ya Lyon wakati huu wa dirisha la usajili na kocha huyo amemsifu kwamba ni mtu mpya mwenye athari kikosini.

“Nadhani alicheza vizuri,” Koeman alimuongelea Memphis.

“Ni mchezaji mwenye ubora na alionesha hilo.

“Ni mchezaji muhimu kwetu kwa sababu tunataka kuwa na ushindani mbele.”

Koeman Ampa 5 Depay Baada ya Mechi ya Kwanza na Barca

Wote ambao walikuwa wakitizama kwenye Televisheni hawakuwa na mchana mwepesi kutokana na jezi mpya za Barcelona za zambarau zililochanganyika na rangi nyekundu, bluu na nyeupe za Girona, lakini kutokana na kile Koeman aliweza kuona aliridhika nacho.

“Tulikuwa na mzuka zaidi kuliko siku nyingine,” Koeman alisema

“Girona ni timu nzuri inayojaribu kucheza. Ulikuwa mchezo mzuri, ikizingatiwa bado tuko katika maandalizi ya msimu. Kulikuwa na burudani kwa pande zote mbili.


FURAHIA KASINO MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Kasino ya Mayan Eagle inakukufanya kuwa bingwa wakati wowote unapoamua kuicheza. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa