Baada ya kusambaa taarifa zinazojadili hatma ya Ronald Koeman ndani ya klabu ya Barcelona, kocha huyo ameamua kutoa ya moyoni.

Barca ipo kwenye misukosuko toka mwishoni mwa msimu uliopita, mabadiliko ya uongozi, sakata la Lionel Messi na wachezaji wengine wakubwa kwenye kikosi hicho, kuondoka kwa Quique Setien, matokeo mabaya uwanjani n.k

Kumekuwa na taarifa kuwa aliyewahi kuwa nahodha wa klabu hiyo, Xavi Hernandez anaweza kupewa mikoba ya kukiongoza kikosi hicho kuanzia msimu ujao. Hili linachagizwa na kauli ya Raisi wa Barca, Joan Laporta kuwa mwishoni mwa msimu huu kutakuwa na mabadiliko makubwa kwenye klabu hiyo.

Koeman ameamua kutoa ya moyoni kwa vyote vinavyoendelea ndani ya klabu hiyo na miongoni mwa wanahabari nchini Hispania. Akizunguzia kinachoendelea, Koeman anasema:

” Unahitaji kuwaheshimu zaidi wachezaji na kocha wako. Mwishoni mwa msimu, sijauona msaada wa klabu.

“Vitu vinatokea kwenye vyombo vya habari. Haikupaswa kuwa namna hiyo, kuna namna nyingine ya kufanya vitu. Ninajua hapa kumekuwa na msukumo mkubwa na ninakubaliana na hilo.

“Lakini ninadhani kwenye hii nchi, kumekuwa na utamaduni wa vyombo vya habari kujihusisha na hatma za makocha, ninadhani hii sio heshima. Kiukweli, sijui kama nitaendelea kuwa kocha. Sijazungumza na raisi.

“Ninajua tunapaswa kufanya mabadiliko ili kushinda mataji na kama hiyo inamaanisha kuwa na kocha mpya au wachezaji, yote sawa, lakini tunapaswa kupewa taarifa.”

Barcelona chini ya kocha huyu, wameshinda taji la Copa del Rey, wanamaliza msimu wakiwa nafasi ya 3 kwa mara ya kwanza tangu 2007/2008 na walitolewa kwenye 16 bora kunako Ligi ya Mabingwa baada ya kufungwa nje ndani na PSG.


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

River Plate, River Plate, Enzo Perez Aonesha Uwezo Golini., MeridianbetBASHIRI SASA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa