Shirikisho la soka duniani (FIFA) imetangaza miji itakayotumika katika michuano ya kombe la dunia la wanawake mwaka 2023. New Zealand na Australia ndio nchi zilizotajwa kama wenyeji wa michuano hiyo. Hii ni mara ya kwanza kwa michuano mikubwa ya kidunia kuchezwa katika nchi mbili tofauti, ikijumuisha jumla ya miji tisa.

Michuano hii mikubwa duniani inategemewa kujumuisha timu 32, hii itakuwa ni tofauti na vile ilivyokuwa mwaka 2019, ambapo kulikuwa na timu 24 huko Ufarasa.

FIFA wamesema wamelazimika kuongeza idadi ya timu kutokana na maendeleo yaliyoonekana wakati wa michuano ya kombe la dunia la wanawake la 2019 nje na ndani ya uwanja.

“Kutokana na mafanikio makubwa yaliyotokana na mafanikio ya ufaransa 2019, Kombe la Dunia la wanawake la FIFA mwaka 2023 litahusisha miji tisa katika nchi za Australia na New Zealand” Rais wa FIFA Gianni Infantino alisema katika tamko rasmi la shirikisho hilo.

Licha ya FIFA kutangaza miji hiyo tisa, ikianzia huko Auckland katika uwanja wa Eden Park na fainali ya michuano hiyo inategemewa kufanyika katika Uwanja wa Australia, huko Sydney.


UNAWEZAJE KUKOSA KASINO YA BREAK AWAY LUCKY WILDS INAYOKUPA NAFASI YA USHINDI MURUA.

Break Away Lucky Wilds ni moja ya Sloti pendwa katika kasino za #meridianbet inayokupa mara 11,000X ya dau lako, unayo nafasi ya kuwa milionea unasubiri nini?

Kombe, FIFA:Australia na New Zealand Mwenyeji Kombe La Dunia la Wanawake 2023, Meridianbet

CHEZA HAPA

6 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa